Narok Pombe

Maafisa wa usalama kutoka serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na idara mbalimbali za usalama kaunti ya Narok, wameanzisha operesheni kali ya kupambana na ugemaji, usambazaji, uuzaji na hata unywaji wa pombe haramu pamoja na matumizi mengine ya mihadarati katika kaunti ya Narok.

Viongozi wa Narok wakiongozwa na Gavana Patrick Ntutu na Kamishena Isaac Masinde, wameahidi kuunga mkono juhudi hizi ili kutokomeza uraibu wa dawa za kulevya katika kaunti ya Narok.Gavana Ntutu ameelez akwamba serikali ya Kaunti imekuwa ikitoa leseni kwa wauzaji wa vileo, ila amewaonya wale waliotumia fursa hiyo kuuza vileo karibu na maeneo ya shule au katika maeneo ambapo wananchi wanaishi.

Zaidi ya hayo Ntutu ameahidi kuwakabili wote wanaoendeleza uuzaji wa vileo ghushi na pombe haramu, akitaja kwamba vijana kati ya umri wa miaka 18-25 ndio wanaoathirika zaidi na pombe hizi.

Kwa upande wake, kamishena Isaac Masinde amesisitiza mpango wa serikali kuu wa kulikabili kero la pombe haramu akiahidi kuanzishwa kwa operesheni kali ili kuwakamata wauzaji wa mihadarati mjini Narok. Viongozi hao walizungumza mjini Narok baada ya kuandaa kikao na washikadau wengine walio katika mstari wa mbele kukabiliana na pombe haramu.

https://twitter.com/OleNtutuK/status/1671168148983402496?s=20

June 20, 2023