BY ISAYA BURUGU,13TH JUNE,2023-Washukiwa wanne wa ujambazi wameauawa kwa kupigwa  risasi leo asubuhi katika nyumba moja huko Kijipwa eneo la Takaungu kaunti ya Kilifi.

Wakati wa kisa hicho, maafisa wa usalama walifanikiwa kupata bunduki aina ya AK47 kutoka kwao.Kwa mjibu wa polisi ni kwamba,Bunduki hiyo ilikuwa na risasi saba wakati ikipatikana.

Washukiwa hao ambao wote ni wanaume wanahusishwa na msururu wa wizi ambao  umekuwa ukiripotiwa  kaunti za Machakos,Kwale na Mombasa ambapo pesa zimepota.

Washukiwa hao waliouawa wanajumuisha  mshukiwa aliyekuwa akisakwa na polisi kuhusiana nak isa cha wizi wa duka la MPESA jijini Mombasa mwezi Feburuari mwaka huu aliyenaswa kwenye kamera za CCTV.

 

 

 

June 13, 2023