Wabunge kutoka jamii za wafugaji wamekubali kuweka tofauti zao kando na kushirikiana na serikali ili kumaliza ukosefu wa usalama na migogoro inayohusiana na wizi wa mifugo katika eneo la Kaskazini mwa bonde la Ufa.
Viongozi hao wametoa wito wa kusitishwa mapigano na mizozo ya mifugo Pamoja na mauaji yanayohusiana na mizozo hii.
Wakiongozwa na mbunge wa Saku Dido Raso, wabunge hao wameeleza imani yao kwamba ushirikiano wao utazaa matunda katika kusitisha mapigano hayo.