BY ISAYA BURUGU,16TH MARCH,2023-Kabla ya kuandaliwa  kwa mandamano yaliyopangwa jumatatu ijayo jijini Nairobi,wabunge wanaoegemea mungano wa Azimio bungeni wametoa orodha ya maswala yanayowakera  chini ya serikali ya Kenya Kwanza.

Azimio chini ya uongozi wa kinara wake Raila Odinga  umekuwa ukiendesha  msururu wa mikutano ya umma kuwaraia wananchi kukatalia mbali  serikali ya Ruto wanayoitaja kama isiyokuwa halali.

Wanasema serikali imefanya Maisha kwa mwananchi wakawaida kuwa ngumu wakitaja kupanda kwa gharama ya Maisha.MASWALA wanayosema yanawakera ni Pamoja na gharama ya juu ya Maisha,

ubaguzi katika ugavi wa fursa za ajira za serikali,kunadi kenya kwa watu binafsi,wanataka TUME ya IEBC kufungua sava,wanakataa mchakato wa kuunda upya tume ya IEBC,kutatiza mkondo wa kidemokrasia na uongozi usioweza .

 

 

 

 

 

March 16, 2023