Wafanyabiashara mjini Kilgoris Trasmara magharibi wamefanya maandamano kulalamikia hatua ya kaunti ya Narok kuwatoza ushuru kila wakati.
Wakizungumza na waandishi wa habari wafanyabiashara hao wamesema imekuwa vigumu sana kwao kufanya kazi kwani serikali ya kaunti ya Narok huwaitisha ushuru kila wakati hatua ambayo wanasema imechangia kudorora kwa uchumi katika soko hilo.
Kando na hayo wafanyabiashara hao wamelalamikia muundo msingi mbovu katika soko hilo hali ambayo husababisha wafanyabiashara kunyeshewa wakati wa mvua.
Mbunge wa Trasmara magharibi Julius Sunkuli aliingilia kati na kuhaidi kuwasilisha malalamishi yao kwa serikali ya kaunti huku akidai wakati umewadia wa Wafanyibiashara kupewa heshima kwa kuboresha mazingira yao ya kazi.