BY ISAYA BURUGU 18TH MAY 2023-Wafanyikazi wa Chuo Kikuu cha Maasai Mara chini ya mwavuli wao (KUSU) wamemuomba Waziri wa elimu Ezekiel Machogu kuchukua hatua za kisheria kufuatia madai ya uvujaji wa fedha na ukandamizaji wawafanyikazi wa chou hicho unaodaiwa kuendeshwa na usimamizi.

kupitia mkurugenzi wao mkuu ambaye pia ni katibu wa tawi la Kaunti ya  Narok Galfin Omuse aliomba waziri ya elimu kutekeleza maelewano ya 2017- 2021 almaruf CBA ambayo imetekelezwa katika vyuo vikuu vingine na kufuatia uamuzi wa mahakama ya Nakuru iliyoamua kuwa walipwe.

Omuse anadai  kuwa mawakili wanaowakiwakilisha chou kikuu  hicho wamejiunga na uongozi kupinga uamuzi wa kesi hiyo kwa malipo yao ya shilingi milioni 60 huku akidai kuwa tayari milioni 30 na ambazo zingetumika kulipa deni wanalodai zimelipwa kupitia njia gushi.

Omuse pia alidai kuwepo madai ya vitisho kwa maisha yake kuwa atapigwa risasi kufuatia malalamishi hayo akiapa kutonyamaza kamwe.Aliyazungumza haya nje ya afisi za chuo hicho huku ambapo pia alidai kutokuwepo kwa baraza la chuo hali ambayo imeathiri utendakazi kwa miaka mingi kwani naibu Kansela na Naibu wake wamekuwa katika mikataba ya kaimu huku wakiapa kusimama kidete kwa siku zijazo ambazo Chacha amesalia kabla kustaafu rasmi.

May 18, 2023