BY ISAYA BURUGU,14TH JUNE,2023-MAHAKAMA ya Shanzu imefahamishwa kwamba wafuasi 16 wa mafundisho ya mhubiri Paul Mackenzie hawajakuwa wakila tangu Juni 4, 2023.

Kiongozi wa Mawakili wa Upande wa Mashtaka Jami Yamina amesema ni Mackenzie tu na mshukiwa Smart Mwakalama ambao wamekuwa wakibomoa mlo.

Washukiwa wengine waliosalia walianza mgomo wa kususia mlo siku 10 zilizopita – tangu Juni 4, 2023 – ambapo wamekataa kula chakula na kunywa maji.

Mackenzie na washukiwa wengine 17 wanadaiwa kuwashawishi waumini kufuata mafundisho ya kupotosha.

Waumini wa dhehebu la Good News International waliaga dunia kwa mamia baada ya kulemewa na makali ya njaa wakiwa kwenye mfungo katika msitu wa Shakahola.

 

 

 

 

June 14, 2023