BY SAIAYA BURUGU 26TH JULY 2023-Ibaada maalum inaandaliwa hivi leo katika kanisa katoliki la Christ the king mjini Nakuru kuwakumbuka waadhiriwa wa mauaji katika mandamano ya wiki iliyopita Nakuru magharibi. Muungano wa Azimio ulisitisha maandamano ya leo huku Wafuasi wa Azimio wakitakiwa kuwakumbuka waathiriwa .Viongozi wa Azimio pia wamepanga kuwatembelea waathiriwa hospitalini ambapo Wafuasi wa Azimio watakUwa wakiwasha mishumaa na kukesha.Huyu hapa Asumpta Wangui ambaye ni mwenyekiti wa Azimio kaunti ya Nakuru.
Aidha baada ya ibaada hiyo wafuasi wa Azimio watawatembelea waadhiriwa wengine waliopata majeraha ambao wangali wanapokea matibabu hospitalini.
Wakati huo huo Gavana wa kaunti ya Homabay Gladys Wanga hivi leo ameongoza hafla ya kuwasha mishumaa ufuaoni mwa ziwa Victoria kuwambuka waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa mandamano yaliyopita ya Azimio.Wakati wa hafla hiyo ,gavana Wanga ametangaza kuwa serikali ya kaunti yake itagharamia mazishi ya waliouawa saw ana kulipa gharama za matibabu kwa waliojeruhiwa ambao wangali wamelazwa katika hospitali mbali mbali.
Katika kaunti ya Kisii wafuasi wa Azimio la umoja wamemiminika katikakati ya mji wa Kisii wakiimba na kuwasha mishumaa kuwakumbuka waadhiriwa wa mashambulizi kutoka kwa polisi wanaoripotiwa kuuawa na hata kujeruhiwa kwenye mandamano.