BY ISAYA BURUGU 29TH JUNE,2023-Wahudumu kwenye sekta ya uchukuzi mjini Ilbisili kaunti ya Kajiado wanalalamikia kuongezeka kwa ajali zinazosababishwa na malori ya masafa marefu ,huku hatua dhidi ya wahusika ikikosa kuchukuliwa.

Wahudumu hao walilizuia lori lililosababisha ajali katika Barabara ya  Namanga  wakilalamikia kisa cha hivi punde Zaidi ambapo mmoja wao aligongwa lililokuwa likiendeshwa kwa kasi na kufariki.

Wanadai mmiliki wa lori hilo alikuwa anapanga kuliondoa lori lake katika kituo cha polisi wakihofia kuwa huenda haki ikakosa kutendeka.

Wanaitaka idara ya usalama haswa katika Barabara kuu ya Namanga kuajibika wakidai kuwa tangu mwaka 2021 zaidi ya watu 20 wakiwemo madereva wa matatu wamefariki.

 

 

 

June 29, 2023