BY ISAYA BURUGU 21ST APRIL,2023-Waislam wengi humu nchini wanasherehekea  Eid al Fitr  kuashiria kukamilika rasmi kwa mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhan.

Maelfu ya waumini wakislam wamekongamano katika maeneo  mbali mbali ya kuabududia na viwanja kote nchini nyakati za asubuhi kwa maombi maalum ili kuanzisha sherehe hizo.

Hii ni baada ya mwezi mpya kuonekana  katikas ehemu mbali mbali nchini jana usiku zikiwemo eneo la pwani na kaskazini amshariki.Waislamu hufuata kalenda la lunur wala sio ile ya Solar.

Hata hivyo Eid haiko kwenye tarehe rasmi lakini hutegemea na ule wakati mwezi unapoonekana na kuashiria kukamilika kwa mwezi wa Ramadhan na kuanza kwa mwezi wakislamu wa Shawwal.

Kule Mombasa baadhi ya viongozi wa dini ya kislam wamelezea furaha yao kufuatia kikamilika kwa Ramadhan na kumuomba mungu kuendelea kubariki nchi hii na kuingilia kati changamoto mbali mbali zinazoikumba.Pia wameomba kuwa rehema za mungu zishukie taifa la Sudan ambalo linakumbwa na vita.

 

 

April 21, 2023