BY ISAYA BURUGU 19TH JUNE,2023-Wakaazi wa kijiji cha Motony wadi ya Mara Narok Magharibi wameshiriki maandamano kupinga ujenzi wa bara bara ya upana wa mita 50 itakayopita katika shamba la jamii.Wakiongozwa na Christopher Samoei wakaazi hao waliojaa hamaki walibeba matawi wakidai bara bara hiyo inayonuiwa kutoka Ronge hadi Motony almaruf CIS MARA /LEMEK/51 ilipewa shilingi milioni 5 na Kaunti ya Narok na huenda ukamilisho wake ukazua vita baina ya jamii zinaoishi hapo.
. Aidha Samoei ameiomba serikali kupitia waziri wa ardhi ya Kaunti ya Narok na afisi ya DCI kuingilia kati na kusitisha ujenzi huo.Nicholas Busienei ambaye ni mzaliwa wa eneo hilo anakiri kuwa eneo hilo lilitengwa kwa malisho ya wanyama,ukuzaji miche miongoni mwa zingine na mababu wao.
Eneo hilo linadaiwa kumilikiwa kinyume na sheria na makansela wawili hadi mwaka wa 1995 ambako walilisalimisha kwa kundi la kibinafsi la Sugutekap Motony kilichowalazimu wakaazi kununua hekari 10 licha ya shamba hilo kuwa la uma.