Mamia ya wakaazi mjini Narok walifaidika na Uchunguzi wa afya pamoja na hamasisho ya bure kuhusu ugonjwa wa saratani kutoka kwa wahudumu wa afya wa hospitali ya rufaa ya Narok, hospitali ya Medicatia kwa ushirikiano na kanisa la New Seventh Day Adventist.
Shuguli hiyo ya siku moja iliyofanyika katika uga wa William Ole Ntimama ilijumuisha kupewa mawaidha ya kiafya jinsi inavyohitajika kisha kufanyiwa vipimo tofauti.
Akizungumza baada ya zoezi hilo Mourine Makori ambaye ni muuguzi katika hospitali ya rufaa ya Narok alisema zoezi hilo liliafikiwa kufuatia ongezeko la maambukizi ya saratani hivyo basi kukawa na haja ya kuandaa shuguli hiyo.
Douglas Mbaka msimamizi wa mauzo katika hospitali ya kibinafsi ya Medicatia aliunga mkono haja ya kila mtu kufanyiwa uchunguzi wa mapema ili kubaini iwapo wanaugua saratani.