BY ISAYA BURUGU 26TH JAN,2023-Risala za rambirambi kwa jamaa ndugu na marafiki wa Mwenda zake aliyekuwa Waziri wa elimu Prof George Magoha zinazidi kutolewa  siku mbili baada ya kifo chake.Wakaazi wa kaunti ya Narok wamelezea masikitiko yao kuhusiana na kifo hicho cha ghafla wanachodai kimelipokonya taiafa hili mtu aliyewajali Watoto wa Kenya na kuwapigania kupata elimu bora kupitia fursa alizopata kuhudumu katika sekta ya elimu.

Hususan wanakambuka jinsi Magoha alivyopigania Watoto kusalia shuleni hata wakati wazazi hawakuwa na uwezo wa kulipia karo katika nyakati tofauti.

Aidha wanamtaka Waziri wa elimu Ezekiel Machogu kuiga mfano wa mwendazake Magoha wa kutetea maslahi ya mtoto wa Kenya na kuendeleza mageuzi kwenye sekta hiyo yaliyoanzishwa na Magoha.

 

 

 

 

 

 

 

January 26, 2023