Clement Kiarie, dereva wa basi la abiria lililohusika katika ajali eneo la Twin Bridge mnamo Jumanne, Januari 7, ameshtakiwa.

Kiarie, ambaye pia anajulikana kwa jina la Taylor, alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Molo Daisy Mosse leo asubuhi ambapo alishtakiwa kwa makosa 15 ya kusababisha kifo, 1 la kukiuka matumizi ya bima, kuendesha gari kwa uzembe na shtaka lingine la kubeba abiria 41 wasio na bima.

Hata hivyo alikanusha mashtaka na kuachiliwa kwa bondi ya Ksh.1 milioni.Siku ya Jumanne, basi la umma ambalo Kiarie alikuwa akiendesha lilihusika katika ajali ya barabarani iliyogharimu maisha ya watu 15 katika eneo la Twin Bridge, kwenye barabara kuu ya Nakuru-Eldoret.

Alikamatwa Jumatano na kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Mau Summit.Kesi hiyo itatajwa Januari 29, 2024.

January 11, 2024