Uhusiano mzuri kati ya Kenya na Ujerumani umeendelea kuimarika kufuatia Ziara ya Kiserikali ya Kansela Olaf Scholz siku ya Alhamisi.

Katika mkutano wa pande mbili na mkutano na wanahabari katika Ikulu ya Nairobi, Rais William Ruto alitoa wito wa kupunguzwa kwa vikwazo vya uhamiaji ili Wakenya waweze kupata nafasi za kazi katika nchi hiyo ya Ulaya.

Chansela Scolz alikubali kufungua milango kwa Wakenya 250,000 wenye taaluma, ujuzi katika juhudi za kutimiza mahitaji makubwa ya kazi ya Ujerumani.

Viongozi hao wawili pia walikubaliana juu ya hitaji la ulimwengu kufanya kazi kwa pamoja katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

 

May 5, 2023