Kaimu mkurugenzi mkuu katika wizara ya afya dkt. Patrick Amoth amewahimiza wakenya kutokuwa na hofu kufuatia wimbi la saba la ugonjwa wa korona unaoshuhudiwa humu nchini. Akizungumza na waandishi wa habari, Amoth amesema kuwa hakuna haja ya kurejesha vizuizi vya kukinga ugonjwa huo ikizingatiwa kwamba takwimu zilizotolewa hivi majuzi sio za kitaifa.
Aidha Amoth ameendelea kutoa wito kwa wale ambao hawajapokea chanjo ya korona kutembelea vituo vya afya na kupokea chanjo hiyo.
Hivi karibuni idadi ya maambukizi ya korona imekuwa ikiongezeka kila kuchao. Aidha wataalam wa afya wanaochunguza magonjwa yanayosambaa, walisema kuwa aina hii ya kirusi cha korona haina madhara kama vile aina ya delta.