BY ISAYA BURUGU,12TH NOV 2022-Wakfu wa KCB na shirika la kimaendeleo la ujerumani hivi leo imesambaza vifaa 476 vya ujenzi kwa vijana katika sekta ya ujenzi vinavyogharimu shilingi milioni 19 .
Hii ni kufuatia kukamilishwa kwa mafunzo ya kiufundi kwenye baadhi ya taasisi zilizoidhinishwa kote nchini.Haya ni kulingana na ushirikiano kati ya mashirika hayo mawili kwa lengo la kuongeza uwezo wa vijana hao kuajiriwa na kuwapa pato vijana 3500 katika sekta ya ujenzi.
Mpango huo unatarajiwa kujaza pengo lililoko kati ya vijana wanaosaka ajira na na ujuzi wa kiufundi unaozidi kuhitajika.Kuanzia mwaka ujao vijana wanaopata ujuzi kama huo kutoka kwa kundi hilo watapokea masharti rahisi kuanzisha biashar zao chini ya mpango wa huduma za kibiashara wa wakfu wa KCB hadi biashara zao zisimame.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ,Mkurugenzi wa ushirikiano kwa benki ya KCB Esther Waititu amesema kuwa benki hiyo inaendeshwa na moyo wa kufanikisha biashara kama njia moja ya kutoa suluhu kwa changamoto zinazokumba jamii.