Viongozi wa Narok wakiongozwa na gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu walilazimika kuingilia kati na kuzungumza na wakulima wa ngano kusitisha mandamano yao baada ya shuguli za usafiri kutatizika katika barabara kuu ya Narok-Bomet kufuatia  kufungwa kwa zaidi ya masaa manne na wakulima hao.
Gavana Ntutu akiandamana na mbunge wa Narok kaskazini Agnes Pareyio na kiongozi wa kina mama kaunti ya Narok Rebecca Tonkei waliwarai wakulima hao kufungua barabara ili kuruhusu wasafiri kuendelea na safari zao kuelekea sehemu mbalimbali.
Kwa upande wao,wakulima hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Stanley Koonyo, wamelalama kwamba serikali imechukua muda mrefu kutatuliwa huku zaidi ya gunia elfu mia nne kusalia kwenye maghala kwa muda wa miaka miwili kufikia sasa.
February 24, 2025

Leave a Comment