Wanafunzi Machogu

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, amewataka walimu wakuu kote nchini kuhakikisha kwamba shughuli za masomo zinaandaliwa kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi kasorobo alasiri kila Jumatatu hadi Ijumaa.

Akizungumza alipokutana na wakuu wa muungano wa walimu wakuu wa shule za upili nchini, Waziri Machogu ameeleza kwamba shughuli za masomo zinafaa kutekelezwa kwa muda wa saa sita pekee, ili kuwawezesha wanafunzi kuwa makini kuhusu kile kinachofunzwa, na pia kuwaruhusu wanafunzi kujihusisha na shughuli zingine za ziada.

Katika kikao hicho wakuu wa muungano wa shule za upili nchini wakiongozwa na mwenyekiti Bw. Indimuli Kahi waliiomba wizara hiyo kuangazia maswala mbalimbali ya muhimu ambayo yamekuwa yakitatiza shughuli za masomo katika shule mbalimbali, yakiwemo maswala ya kuchelewa kwa fedha za kusimamia shughuli za mtaala mpya wa CBC.

June 16, 2023