Wanafunzi tano wa shule ya upili wameaga dunia adhuhuri ya leo, baada ya matatu walimokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali mbaya katika eneo la Delamere, Naivasha kwenye barabara kuu ya Nakuru-Nairobi.

Wanafunzi hao kutoka Shule ya Upili ya Wasichana ya Mbihi iliyo katika kaunti ya Vihiga walikuwa kati ya wasafiri 11 waliokuwa katika matatu hiyo iliyokuwa ikitoka Nakuru kuelekea Nairobi.Taarifa zinaeleza kwamba dereva wa matatu alipoteza mwelekeo baada ya kugongana ana kwa ana na lori lililokuwa likitoka upande tofauti alipokuwa akijaribu kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake.

Tano hao walifariki papo hapo, huku wengine 7 akiwemo dereva wa matatu wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Naivasha Level Four ili kupokea huduma za matibabu.

April 18, 2023