BY ISAYA BURUGU 6TH FEB,2023-Zaidi ya wanafunzi 800,000 wa kidato cha 1 wameanza kujiunga na shule mbali mbali za upili kote nchini hivi leo.Ni wiki mabyo pia walimu 30,000 walioajiriwa wanatarajiwa kuripoti mashuleni.Tume ya kuwajiri walimu nchini ilisema 10,000 kati ya walimu hao wataajiriwa kwa masharti ya kudumu na ya uzeeni huku 25,550 watakuwa katika kandarasi.
Tume hiyo ilisema nafasi 9,000 ni za walimu wa kudumu wa shule za sekondari na 1,000 za walimu wa shule za msingi, wakati nafasi 21,550 ni za walimu kwa shule za sekondari za chini.Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti, wizara tayari imesambaza vitabu vyao vya kusoma.Mnamo Ijumaa, Katibu wa Kudumu wa Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi Belio Kipsang alithibitisha kuwa shule tayari zimepokea vitabu hivyo.
Muhula mpya wa kidato cha kwanza unaanza huku kukiwa na sheria kali za kuwazuia wakuu wa shule ‘kuwadhulumu’ wazazi.
Wizara imeweka hatua kadhaa kuhakikisha udahili wa wanafunzi ni laini.Hii ni pamoja na agizo la sare na ada za ziada; sare zote lazima gharama sawa. Ushuru wa ziada ni marufuku bila idhini.