Wanafunzi waliofanya mtihani wa kitaifa KCSE mwaka jana sasa wanaweza kujisali kupata nafasi katika vyuo vikuuu humu nchini.
Akizungumza alipokuwa akizindua shuguli ya uteuzi wa wanafunzi kupitia njia ya mtandao KUCCPS, waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alisema wanafunzi 173,127 waliopata alama ya C+ na Zaidi watajiunga na vyuo vikuu huku waliopata alama ya chini wakisajiliwa kujiunga na Vyuo vya kiufundi.
Machogu pia alisema kuwa taasisi zote tayari zimetimiza masharti yote yanayohitajika kusajili wanafunzi na tayari zimechapisha ada za kozi kwenye tovuti zao.
Baada ya kuchaguliwa, Waziri Mkuu alisema, wanafunzi watapewa fursa ya kutuma maombi ya ufadhili wa masomo ya serikali kutoka kwa hazina ya Chuo Kikuu kulingana na mtindo mpya wa ufadhili uliotangazwa na Rais William Ruto.
Aidha udhamini huo wa serikali utastahiki tu wanafunzi ambao watajiunga na vyuo vikuu vya umma na sio wale wanaochagua vyuo vikuu vya kibinafsi.