BY ISAYA BURUGU 29TH DEC 2022-Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Alshabaab wamewaua watu wawili kwa kuwapiga risasi mapema leo asubuhi katika barabara ya Lamu kuelekea Garsen katika kaunti ya Lamu.
Taarifa zinasema kuwa angalau wanamgambo 10 waliovalia sare za kijeshi walikuwa wameweka kizuizi kwenye barabara hiyo na walikuwa wakiwauliza maswali wendesha magari kabla ya maafisa wakijeshi kuwasii eneo hilo na makabiliano kuzuka.
Uvyatulianaji mkali wa risasi kati ya wanamgambo hao na wanajeshi ulizuka kabla yao kutorokea katika msitu wa Boni. Maafisa hao walifanikiwa kuwaokoa watu wanne miongoni mwao raia wawili wa Italia waliokuwa wametekwa nyara na wanamgambo hao.
Miili ya watu waliouawa imepelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Mpeketoni huku polisi wakianzisha msako dhidi ya wanamgambo waliotoroka.