BY ISAYA BURUGU 11TH MAY 2023-Kaimu naibu kamishana wa Narok ya kati Aldi Shakur Ali amesema serikali itachuguza wanaotumia mitandao ya kijamii visivyo  na kuwachukulia hatua.Aameyasea hayo alipozungumza na wandishi wa habari katika afisi ya vijana mjini Narok katika mkutano uliyowaleta  pamoja viongozi wa kidini na baraza la wazee ya Jamii ya maasai.

Shakur  amesema kuna baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuzua taharuki  miogoni mwa jamii kaunti ya Narok na idara ya upelelezi wa jinai DCI inafanya uchuguzi.Akidokeza kuwa kwa sasa   idara mbali mbali za serikali zinawafuatilia.

Kauli yake imeungwa mkono na Ali Juma ambaye mwenyekiti wa baraza la Kislamu SUPKEM kaunti ya Narok ambaye amesema kuna haja ya uhusiano kati ya jamii nchini sawa na vyama vya kisasa ili  suluhu ya kudumu ipatikane.

kwa upande wake baraza la wazee ya Jamii ya maasai likiongozwa  na mkurugenzi wa baraza hilo Simion Nchoe amesema baraza hilo linatumia njia mbadala ya kusuluisha kesi mbali mbali kaunti ya Narok. Na kuitaka jamii kutafuta njia ya kuzima mizozo mbali mbali ya ardhi..

 

May 11, 2023