BY ISAYA BURUGU 12TH NOV,2022-Mwakilishi wa akina mama kutoka kaunti hii ya Narok Rebecca Tonkei sasa anawataka wanaume kuwapa Watoto wakike fursa kupata elimu badala ya kuwapachika mimba wakiwa na umri mdogo.
Akizungumza mjini Narok,Tonkei amesema ni ambo la kusikitisha kuona wasichana wengi katika kaunti hii ya Narok wakilazimika kuacha shulle baada ya kupachikwa mimba huku wengine wakiozwa mapema.
Kaunti ya Narok ni moja wapo ya kaunti zinazoongoza kwa ndoa za mapema na watoto wakike kuacha shule kutokana na wanaume wanaowatunga mimba au kuwaoa kwa lazima.Hata hivyo kulingana na Tobkei ni kwamba ni sharti mtindo huo sasa ufike miwsho ili watoto wakike kutoka Narok waweze kufanikiwa maishani kama watoto kutoka sehemu zingine za nchi.
Ametoa wito kwa maafisa wa polisi na serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaume watakaopatikana wakiwaachisha watoto wasichana masomo kwa njia ya kuwapa uja uzito au kuwaoa.