BY ISAYA BURUU 4TH MAY 2023-Askofu wa jimbo katoliki la Ngong John Oballa Owaa hivi leo ameongoza misa maalum kwa ajili ya kuwaweka wakfu  watu wanne kuwa mashemazi.Wanne hao ni Jasper Nyabayo kutoka parokia ya Ichumi kisii,Ambrose misiku kutoka jimbo la kakamega,Joachim Lubobi Kutoka parokia YA Mukumu parish kakamega,na Ronald Rioki kutoka St Anne Kibiku Ngong,

Katika homilia yake baba Askofu amewataka kukumbatia unyenyekevu katika Maisha yao ya kikiristu haswa ikizingatiwa kuwa watapitia changamoto zitakazo kuwa mtihani mkubwa kwa Imani yao.Lakini akawashauri wawe wakumtegemea mwenyezi mungu na pia wafuate kikamilifu kalenda ya jimbo kuhusu mipangilio  mbali mbali kuambatana na mwito wa sinodi ili waweze kutimiza matakwa ya kristu .

Aidha baba askofu akiwasihi mashemazi hao wapaya kuwajongea sana wanyonge watakapokuwa wakitekeleza wajibu wao.Bali na kuwa na hekima kwa askofu wao bila kuhisi kuwa uhuru wao umekanyagiwa na kuhujumiwa.Wamekumbushwa kutojitakia makuu katika kusaka utajiri wa dunia bali wawe na upendo kwa mungu na watu wake katika kumtumikia

.

May 4, 2023