Maafisa wa polisi katika kaunti ya Mombasa wamefanikiwa kuwakamata washukiwa tano wanaodaiwa kuhusika na wizi katika maeneo ya Sargoi na vitongoji vyake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Upelelezi wa Jinai nchini (DCI), maafisa wa polisi walifanikiwa kuwakamata washukiwa hao baada ya kufuatilia matumizi yao ya mtandao wa kijamii wa TikTok. Washukiwa hao walikuwa wakitumia mtandao huo maarufu wa kijamii, kuchapisha video wakionyesha bidhaa mbalimbali walizoiba kutoka kwa wananchi wa eneo hilo.
Following an intelligence led operation, a team of officers based at Central Police Station in Mombasa has arrested five individuals suspected to be members of an organized criminal group that has been operating within Sargoi area and it’s neighborhoods. pic.twitter.com/UAdPDFAfso
— DCI KENYA (@DCI_Kenya) December 6, 2023
Tano hao, ambao wametambulika kama Vincent Ochieng, Shadrack Ochieng, Felix Otieno, Salim Ali, na Shafi Yusuf, sasa wako mikononi mwa mamlaka husika. DCI imebainisha kuwa washukiwa hao watazuiliwa wakati uchunguzi zaidi ukifanyika, na baadaye watafunguliwa mashtaka kulingana na ushahidi uliopo.
The five suspects namely Vincent Ochieng, Shadrack Ochieng, Felix Otieno, Salim Ali and Shafi Yusuf had earlier been captured in a video recording while displaying items that they had stolen from their victims. pic.twitter.com/BcJHWfSAFI
— DCI KENYA (@DCI_Kenya) December 6, 2023