Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ametuma onyo kali kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa wanao eneza semi za chuki na vitendo vya kihuni kwa nia ya kuboronga amani humu nchini.
Katika taarifa yake kwa wakenya adhuhuri ya leo, waziri huyo amesema kwamba wizara yake haiajali mirengo ya kisiasa katika harakati za kudumisha usalama humu nchini. Aidha amekashifu matukio ya uhuni na uvamizi katika shamba la Northlands, akieleza kwamba washukiwa wa kitendo hicho watafikishwa mahakamani hivi karibuni ili kujibu mashtaka.
Kuhusiana na suala la huduma za upatikanaji wa hati za usafiri (Pasipoti) Waziri Kindiki ameahidi kuwa idara ya uhamiaji itaondoa mrundiko ulipo katika kipindi cha siku ishirini na moja zijazo, ili kuwawezesha wakenya wanaohitaji pasipoti hizi, kuzipata katika kipindi cha kati ya saa 24 hadi siku saba.