BY ISAYA BURUGU,4TH OCT,2023-Washukiwa wanne wa wizi wamezuiliwa kwa siku sita na mahakama ya Kerugoya ili kuwapa polisi muda kukamilisha uchunguzi.Wanne hao walikamatwa hiyo jana baada ya kunaswa kwenye kamera ya CCTV wakiwaibia wakaazi wa Kerugoya.

Hakimu mkuu wa Kerugayo Charity Kipkorir alikabali ombi hilo la upande wa mashtaka .Washkiwa hao James Murimi,Jackline Nyakeyo,Paul Macharia na Violet  Wangeci  wataendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kerugoya.

Washukiwa hao walikamatwa na polisi kwa msingi ya Makosa mbali mbali.Mnamo Jumatatu washukiwa hao walinaswa kwenye kamera wakiwashambulia na kuwaibia watu wawili huku wenyeji wakisema wanaishi kwa hofu ya kuvamiwa.Watarajiwa kurejeshwa mahakamani siku ya jumatatu kukabiliana na mashtaka.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

October 4, 2023