Washukiwa watano wa mauaji ya mwanaharakati wa ubasha Edwin Chiloba wataendelea kuzuiliwa kwa wiki tatu zaidi ili kutoa nafasi ya kukamilika kwa uchunguzi.
Tano hao ambapo watatu kati yao hawajahitimu umri wa miaka 18 walifikishwa katika mahakama ya Eldoret. Jacktone Odhiambo ambaye ni mshukiwa mkuu anatuhumiwa kumuua Chiloba aliyepia mwanamitindo.
Aidha Polisi walifanikiwa kulinasa gari linaloshukiwa kutumiwa kuubeba mwili wa Chiloba ambao baadaye ulipatikana umetupwa kando ya barabara.
kikosi cha wachunguzi wa mauaji tatanishi wanatarajiwa kusafiri hadi Eldoret kusaidia katika uchunguzi.Chiloba alipatikana ameuwawa ijumaa iliyopita na mwili wake kuwekwa ndani ya sanduku la nguo na kutupwa huko Kipkaren viungani mwa mji wa Eldoret kaunti ya Uasin Gishu .O
dhiambo alikiri kumuua mwana mitindohuyo kwa madai kuwa alikuwa na mpenzi mwingine.