Watafiti nchini Uganda wamesema virusi vya Ebola vinavyosambaa nchini humo vimebadilika.Prof Pontiano Kaleebu wa Taasisi ya Utafiti wa Virusi vya Ebola aina ya Sudan amesema hata hivyo hakuna ushahidi virusi hivyo vinaweza kuambukizwa zaidi ya aina ya awali.
Kaleebu ameeleza kuwa Walichambua sampuli kutoka kwa kisa cha kwanza kinachojulikana kupimwa wakati wa mlipuko wa sasa ambao umeenea hadi wilaya tano za Katikati mwa Uganda.
Kufikia sasa, kesi 44 zimeripotiwa huku watu 10 wakifa kutokana na ugonjwa huo.Watafiti wanaofuatilia kuenea kwake wamesema maumbile ya virusi hivyo yanafanana na yale yaliyosababisha mlipuko mwingine zaidi ya muongo mmoja uliopita katika eneo hilo hilo. Tafiti zilizofanywa katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinaonyesha kuwa milipuko ya mara kwa mara inaweza kutokea, lakini si zaidi ya miaka miwili baada ya ile ya kwanza kutangazwa kuwa imeisha.
Siku mbili zilizopita wizara ya afya nchini humo ilitangaza kufariki kwa dakatari mwingine kutokana na ugonjwa huo hatari.Bi. Margaret Nabisubi alifariki katika hopitali ya Fort portal baada ya kuugua kwa siku kumi na saba.
Kifo cha Nabisubi kilijiri wiki moja tu baada ya rais wa taifa hilo Yoweri Museveni kusema kuwa hapana haja ya kuweka karantini ikizingatiwa kwamba virusi hivyo havisambai kwa kasi ikilinganishwa na virusi vya korona vinayosababisha ugonjwa wa covid-19.