Wanafunzi milioni 1.2 wa darasa la nane pamoja na wanafunzi milioni 1.3 wa darasa la sita watakaofanya mtihani wa KCPE na KPSEA wiki ijayo wamefanya maandalizi ya mwisho kabla ya mitihani hiyo kuanza.
Watahiniwa hao kutoka shule mbalimbali humu nchini wameonyesha utayari wao hii leo huku walimu wakiwa na Imani wameandaa wanafunzi wao vilivyo.
Wakati huohuo zaidi ya shule mia moja katika kaunti 14 eneo la bonde la ufa zinachunguzwa kwa madai ya udanganyifu kwenye mtihani wa kitaifa huku wanafunzi wakijiandaa kuufanya mtihani huo.
Akizungumza katika mkutano wa kamati ya usalama wa kanda, mratibu wa bonde la ufa Maalim Mohammed amesema kwamba tayari wamepokea ripoti za ujasusi kuhusu udanganyifu huo katika shule kadhaa.
Hata hivyo ameeleza kuwa wameweka mikakati ya kiusalama na kwamba washukiwa watachukuliwa hatua za kisheria