BY ISAYA BURUGU 7TH DEC 2022-Watoto wanne wamelazwa hospitalini wakiwa hali mahututi baada kudaiwa kupewa sumu na kudungwa kisu na baba yao kabla yake kuaga dunia kufuatia kujitia kitanzi.
Kisa hicho kinaripotiwa kutekelezwa kwenye yao ya kukodi katika kituo cha kibiashara cha Nyagoro lokesheni ya Kochia mashariki kaunti ya Homa Bay.
Watoto hao wa kati ya miaka mitatu na tisa walijeruhiwa vibaya na baba yao aliyetambuliwa kama Ronnie Ochieng’ Nyore usiku wa kuamkia leo kufuatia madai ya mzozo wa kinyumbani kati yake na mkewe.Kwa mjibu wa chifu wa lokesheni ya Kochia Mashariki Kennedy Odero aliyefika eneo la tukio,Ronnie aliwadunga kisu tumboni Watoto hao kitumia kisu cha nyumbani baada kudaiwa kuwapa sumu ya kuua wadudu.