Vifo vinavyotokana na ajali za barabarani vimeongezeka mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na mamlaka ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA, watu 1,026 wameaga dunia kati ya tarehe 1 mwezi januari na tarehe 20 mwezi machi kufuatia ajali za barabarani, hii ikimaanisha kuwa vifo kutokana na ajali za barabarani vimeongezeka kwa asilimia 7 ikilinganishwa na vifo 956 vilivyorekodiwa mwaka uliopita.
Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa Watembea kwa miguu wanaongoza kwa vifo kwa 384, ikilinganishwa na 323 iliyorekodiwa mwaka jana.
Wafuatao ni waendesha pikipiki waliorekodi vifo 242 na kuashiria kupungua kidogo ikilinganishwa na 262 mnamo 2023.Mwaka huu, abiria 225 wamepoteza maisha katika ajali za barabarani ikilinganishwa na 170 mnamo 2023.