BY ISAYA BURUGU,4TH DEC,2023-Hafla ya kuadhimisha siku ya watu wanaoishi na ulemavu kimataifa kwenye kaunti ya Narok imeadhimishwa katika shule ya msingi ya Olesankale mjini Narok. Afisa anayesimamia walemavu kaunti ya Narok Julius Ntayia akizungumza katika kwenye hafla hiyo ,bwana Natayia amesema ofisi yake imewahusisha walemavu katika kila sekta ya serikali kuu ya kitaifa.
Ntayia amesema ofisi yake aidha imeshirikiana na wadau mbali mbali kuweka kipaumbele maslahi ya walemavu katika kaunti ya Narok.
Kauli yake Ntayia imeungwa mkono na watu wanaoishi na ulemavu kaunti ya Narok wakiogozwa na Paul Ole Sopia. Sopia amesema ni sharti walemavu wawezeshwe kikamilifu katika juhudi za kukimu matakwa yao katika jamii.
. Usemi uliosisitizwa na Grace Silantoi .Wakati huo huo Mkewe mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi Tessy Mudavadi ameungana na watu wengine wenye mapenzi mema kuadhimisha siku ya kimataifa ya watu wanaoishi na ulemavu nchini.
Bi Mdavadi pia alitumia fursa hiyo kutoa msaada wa chakula kwa watu 400 wanaoishi na ulemavu.
Wakizungumza leo katika uwanja wa shirika la msalaba mwekundu,huko Dagoreti center washika dau mbali mbali wameitaka serikali kubuni mikakati na sera itakayopelekea manusura wa ajali wanasaidiwa.
Hafla hiyo imehudhuriwa na kati ya wengine mbunge wa Dagoret Kusini John Kiarie
.