BY ISAYA BURUGU 4TH OCT,2023-Watu wanne wameuawa usiku wa kuamkia leo huku makumi ya wengine wakiachwa na majeraha kufuatia kuzuka kwa mapigano mapra eneo la Sondu katika mpaka wa kaunti za Kericho na Kisumu.
Wakaazi wa Sondu kaunti ya Kisumu wanaitaka serikali kuingilia kati kufuatia mapigano yaliyosababisha vifo vya watatu Jumanne usiku.
Mapigano hayo yalitokea Jumanne usiku katika mpaka wa Kericho-Kisumu karibu na soko la Sondu.
Wakazi hao wakizungumza na vyombo vya habari siku ya Jumatano walisema wanapata riziki zao kutoka soko la Sondu na kwamba mapigano hayo yamewavuruga shughuli zao za kuwaingizia kipato.
Akidhibitisha kisa hicho kamishna wa eneo la Nyanza Flora Moroa amesema kuwa kisa hicho kilikuwa cha kulipiza kisasi kufuatia kisa cha wizi wa mifugo mnamo siku ya jumatatu kilicho mwacha mtu mmoja akiwa amefariki. Wenyeji wa eneo hilo wamewatuhumu polisi kwa kuzembea katika kukabili hali hiyo,na kumtaka rais Wiliam Ruto kushughulikiwa tatizo la ukosefu wa usalama katika ziara yake ya siku tatu eneo hilo.
Viongozi mbali mbali wakiwemom Gavana wa Kisumu Anyang Nyongo na mwenzake wa Kericho Eric Mutahi wametoa wito wa utulivu huku wakiwataka polisi na wahusika kupewa muda kurejesha hali ya utulivu.