BY ISAYA BURUGU 24TH MARCH,2023-Watu watatu  miongoni mwao maafisa wawili wa polisi  na mfanyikazi mmoja wa halmashauri ya utozaji ushuru ncchini  KRA wametoweka  baada ya mashua walimokuwa wameabiri kuzama ziwa Victoria usiku wa kuamkia leo.

Watatu hao sagenti Anderson Wendot ,kostabo   wapolisi  Onesmus Githinji na mfanykazi mmoja wa KRA  ambaye ni Joseph jillo  aliyekuwa nahodha  wa mashua hiyo wakati mkas ahuo ulipotokea.Taarifa  zasema kuwa watatu hao walikuwa sehemu ya maafisa wanane kutoka vitengo mbali mbali vya polisi vikiwemo,wana maji,opolisi wa utawala, na maafisa wa KRA waliokuwa wakifanya oparesheni,kwenye ziwa hilo wakati mashua hiyo ilipozama yapata umbali wa mita 200 kutoka ufuo wa Mugabo mwendo was aa sit ana dakika 20 za usiku.

Bunduki nne za 4K47 kila moja ikiwa na risasi 30  zilizokuwa na Mohamed,Wendot na Omollo  bado hazijapatikana.Juhudi za kuwasaka maafisa hao zingali zinaendelea.

 

 

 

 

 

March 24, 2023