BY ISAYA BURUGU,24TH MARCH,2023-Waumini wa dini yakislam wamehakikishiwa usalama wa kutosha  eneo la Trasmara magharibi wakati huu ambapo waumini hao  wameanza rasmi kipindi cha mwezi wa mfungo mtukufu wa Ramadhan.Hakikisho hilo limetolewa na  naibu kaunti kamishna wa Trasmara magharibi Ali Hassan Nur.

Nur akizungumza ofisini mwake eneo la Kilgoris Trasmara magharibi amesema serikali imeweka mipango ya kulinda misikiti katika eneo la Nkararu linalokumbwa na  mzozo wa kijamii unaohusiana na utata wa  ardhi .

Nur amesema pia serikali italinda mipaka kati ya Kenya na Tanzania eneo la Ongata Barikoi sawa na eneo la Lolgorian. Naibu huyo wa kaunti kamishna  amewataka wakazi wa eneo hilo kudumisha amani Wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadani.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

March 24, 2023