BY ISAYA BURUGU 23RD MARCH,2023-Waumini wa dini ya Kislamu kote nchini hivi leo wameungana na wenzao duniani kuanza kipindi cha mwezi wa mfungo mtukufu wa Ramadhani.Katika kipindi hiki,waislam hufunga, kusali, na kutoa msaada kwa wasiojiweza katika jamii.
Mkuu wa maimamu kaunti ya Uasin Gishu Shelkh Abubakar Bini ametoa wito kwa uongozi wa kisiasa nchini kuhakikisha kuna mazingira yenye amani kuwawezesha waumini wa dini ya kislamu kuwa na wakati bora kipindi hiki cha Ramadhani.
Hususan Shekh Bini anatoa wito wa kuwepo mazungumzo na viongozi wa upinzani kusitisha mandamano yanayoendelezwa na mungano wa Azimio la umoja. Vilevile amelezea haja iliyoko kwa serikali kutatua swala la gharama ya juu ya kimaisha.