BY ISAYA BURUGU ,17TH JUNE,2023-Naibu kamishana wa Narok magharibi Derusis Muyesus ametoa wito kwa wenyeji wa eneo hilo kuhakikisha watoto wao wamepata elimu.

Akizungumza eneo la Lemek Narok magharibi katika hafla ya  madhimisho ya mtoto wa kifrika yaliyoandaliwa jana,kamishana huyo amesema elimu pekee ndio ufunguo wa maisha na kuwataka wenyeji wa eneo hilo kujiepusha na  mila potovu hasa ukeketaji mimba za mapema na ndoa za mapema ambazo zimepelekea idadi ya juu ya wasichana kukosa elimu.

Muyesu wakati uo huo amesema mitandao ya kijamii imepelekea wanafunzi wengi kupotoka maadili.

. Kauli ambayo imeungwa mkono na Agness Ngeno ambaye anayesimamia maswala ya kijinsia kaunti ya Narok.

Ngeno amesema wazazi wengi wamewapa wanao simu hatua ambayo amesema imechagia kudorora kwa maadili kwa wanafunzi wengi kwa kutazama picha na mambo yasiyofaa.

 

 

 

 

June 17, 2023