ecitizen

Wizara ya teknolojia na mawasiliano nchini imedhibitisha taarifa kuwa wadukuzi walijaribu kupenyeza ndani ya Tovuti ya E-Citizen inayotumika katika utoaji wa huduma za serikali.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyochapishwa alasiri ya leo na waziri wa mawasiliano nchini Eliud Owalo, wadukuzi walijaribu kupenyeza kwenye tovuti hiyo juma moja lililopita, jambo ambalo lilichangia kupungua kwa kasi ya huduma kwa wakenya wanaotumia tovuti hiyo.

Katika taarifa yake, waziri Owalo hata hivyo ameeleza kwmaba mtandao huo ungali salama, huku asasi zote zinazohusika zikiendelea kuimarisha usalama na kutoa huduma kwa wananchi. Taarifa yake pia ilifuatia taarifa kutoka kwa idara ya mambo ya nje iliyodhibitisha hitilafu katika mfumo wa utoaji wa e-Visa.

Waziri Owalo katika mahojiano na kituo kimoja cha habari mapema leo, alitoa idhibati kwamba hakuna taarifa zote zilizodukuliwa au kuvuja kutoka kwenye mtandao huo.

https://twitter.com/MoICTKenya/status/1684551656850051073?s=20

July 27, 2023