Waziri wa jinsia na utumishi wa umma Aisha Jumwa kutwa ya leo ameongoza maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kukabiliana na Ukeketaji, kwenye hafla iliyoandaliwa katika eneo la Ntimaru kaunti ya Migori.
Waziri Jumwa alikuwa miongoni mwa mamia ya wakaazi kutoka jamii ya Kuria walioandaa maandamano katika baadhi ya mitaa katika eneo hilo, kuenezeza ujumbe wa kuwarai wanajamii kuacha hulka hii inayowaathiri wasichana.
Maadhimisho haya yaliandaliwa na bodi ya kitaifa ya kupambana na Ukeketaji, baada ya kuongezeka kwa visa vya ukeketaji wa wasichana kati ya wanajamii wa Jamii ya Kuria.
Akizungumza katika hafla hiyo waziri Jumwa ameahidi kuimarishwa kwa vita dhidi ya hulka hii, ambayo sasa imefikia asilimia 9 kutoka asilimia 15 mwaka jana.