KINDIKI KITHURE - Radio Osotua

BY ISAYA BURUGU 20TH JUNE 2023-Waziri wa usalama Kithure Kindiki hivi leo amefika  kufika mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama kuhusiana na utata wa kupandishwa vyeo kwa maafisa wa polisi.

Waziri Kindiki akizungumzia  mzozo wa kupandishwa vyeo kwa  maafisa 500 wa polisi kati ya inspekta mkuu wa polisi Jaapheth Koome na tume ya huduma kwa polisi unaoendelea,amesema swala hilo ni la kisheria na litahitaji usaidizi wa mwanasheria mkuu wa serikali na idara ya mahakama kwa utafusiri haswa ikizingatiwa kuwa utenda kazi wa taaisi hizo mbili ni wakisheria.

Aidha Waziri amekashfu mzozo kati ya Koome na tume ya huduma kwa polisi akisema kuwa mzozo huo unakiuka sura ya sita ya katiba.

.Mzozo huo umendelea kuvutia hisia kutoka kwa wadau mbali mbali wa punde Zaidi ikiwa chama cha wanasheria nchini LSK kinachotaka mzozo huo kusuluhishwa mara moja. Waziri akisema kuwa zoezi la kuwajiri maafisa hao ni sharti lianishwe kwa mjibu wa katiba.

 

 

June 20, 2023