BY ISAYA BURUGU,10TH MARCH,2023-Waziri wa usalama wa ndani Prof Kithure Kindiki amemwagiza mkurugenzi mkuu wa upelelezi wa jinai Mohamed Amin kuharakisha uchunguzi kuhusu kilichopelekea kifo cha kutatanisha cha Geoffrey Mwathi akiwa katika nyumba ya mwanamuziki wa benga wa nyimbo za Agikuyu DJ Fatxo’ mtaani Kasarani mwezi jana.
Kwenye taarifa Waziri Kindiki amemuagiza mkuu huyo wa DCI kuwahusiha watalamu wakuchunguza vifo tatanishi kusaidia kutatua kesi hiyo .
DCI wamedhibitisha kuanza uchunguzi wa kisa hicho.
Mnamo tarehe 22 mwezi jana katika nyumba ya makaazi ya Redwood iliyoko karibu na Safaripark Mwathi wenye umri wa miaka 23 alinaswa kwenye kamera ya CCTV akianguka kutoka Orofa ya kumi kupitia dirisha la nyumba hiyo ya kukodi ya DJ FATXO ambaye jina lake halisi ni Lawrence Njuguna.