KINDIKI KITHURE - Radio Osotua

BY ISAYA BURUGU 26TH APRIL,2023-Waziri wa usalama Kithure Kindiki hivi leo amefika mbele ya bunge la seneti kuangazia baadhi ya changamoto za kiusalama zinazokumba taiafa hili.

Hatua hiyo ya Waziri inajiri huku oparesheni ya kuwaokoa manusura wa janga la dhehebu za Good news international lake Muhubiri bandia Paul Mackenzie kule Kilifi.

Pia kumekuwa na tatizo la muda mrefu la ukosefu wa usalama eneo pana la kaskazini mwa bonde la ufa ambapo kaunti kama vile Elgeyo Marakweti,Samburu,Pokot magharibi , na marsabit zimeahirika.

Hata hivyo Waziri ametetea wizara yake akisema kuwa kufikia sasa mikakati wlaioweka kutatua changamoto hiyo zimeanz akuzaa matunda haswa baada ya visa vya uhalifu na mashambulizi ya majangili kuanz akupungua.

Waziri akisema kuwa upokonyaji silaha kutoka kwa wale wanaozimikili kinyume cha sheria katika maeneo yaliyoadhirika ndio njia ya kipekee ya kupata suluhu.

 

 

 

April 26, 2023