BY ISAYA BURUGU 15TH JULY,2023-Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki  amesema tofauti zote za kisiasa,kiuchumi,kijamii n ahata kidini zinaweza tu suluhishwa iwapo wahusika wote watatumia njia ya sheria.Ghasia na uvunjaji sheria haviwezi kuleta suluhu.

Akizungumza huko Sondu katika mpaka wa kaunti za Kisumu na Kericho eneo ambalo limeshuhudia hali ya taharuki na usalama kuadhirika,amesema waliosababisha ghasia zilizoshuhudiwa eneo hilo siku kadhaa zilziopita hawatasazwa.Waziri amesema serikali iko tayari kuimarisha mbinu za kuleta amani katika maeneo ya mipakani  yalioyokumbwa na mizozo

.Akirejelea mandamano yaliyoitishwa na mrengo wa upinznai ,Waziri Kindiki amesema serikali iko macho kuwakabili watu watakaochochea uharibifu wa mali na uvunjani sheria kupitia njia za kutatiza amani na utulivu wa nchi.

 

 

 

July 15, 2023