BY ISAYA BURUGU,19TH APRIL,2023-Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ametangaza ijumaa wiki hii Aprili 21 kuwa siku kuu yakitaifa kuadhimisha shere ya Idd-ul-Fitr.

Kupitia notisi rasmi katika gazeti la serikali,Waziri Kindiki amesema hatua hiyo inambatana na mamlaka aliyo nayo  chini ya kifungu cha pili sehemu ya kwanza cha katiba.Sherehe ya Eid al-Fitr, ambayo inashiria kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan ni siku muhimu sana kwa waumini wakislam.

Sherehe hiyo huadhimishwa kufuatia kukamilika kwa siku 29 au 30 za kufunga na kuomba tangu asubuhi hadi jioni katika mwezi wa mfungo mtukufu wa Ramadhan.

 

April 19, 2023