Waziri Kindiki

Serikali ya kitaifa kupitia kwa wizara ya usalama wa ndani inapania kuboresha huduma za magereza na kuhakikisha kwamba vituo hivi vya urekebishaji vinasaidia kutekeleza wajibu wake kwa njia inayofaa.

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki alitangaza haya alipozuru gereza la Mwea, akisema kwamba wizara hiyo imeandaa mwongozo wa mageuzi katika idara ya magereza, mageuzi ambayo yataanza kutekelezwa mara tu baada ya kuidhinishwa na baraza la mawaziri.

Waziri huyo pia ameeleza kwamba wizara yake inapania kufanyia marekebisho sheria zinazosimamia idara za urekebishaji wa tabia katika kipidi cha miezi tatu iyayo.

https://twitter.com/InteriorKE/status/1655562338664079361?s=20

SOMA PIA: Serikali kutoa shilingi bilioni moja kufanikisha mageuzi magerezani nchini asema waziri Kindiki

May 8, 2023