BY ISAYA BURUGU 10TH APRIL,2023-Waziri wa uchukuzi na miundo msingi Kipchumba Murkomen amesema kuwa serikali haijafilisika  bali inakabiliana na mzogo mzito wa madeni ilijipata ndani kutoka kwa utawala wa serikali ya awali ya Jubilee.Kwa mjibu wa Murkomen ni kwamba deni hilo ni kubwa na sio rahisi kwa serikali yoyote kubeba uzito ulioko.

Akionekana kuitetea serikali kutokana na madai ya kutoweza kuwalipa wafanyikazi wa umma kwa wakati,Murkomen ameipongeza serikali ya rais Wiliam Ruto akisema kuwa iko katika mkondo unaofaa kukabili hali hiyo .

Wiki iliyopita,taarifa za wafanyikazi wa umma kutolipwa mshara wa mwezi jana kwa wakati ziliibuka huku walioadhirika Zaidi wakiwa  maafisa wa mashirika ya umma.

Magavana pia wamelalama kuwa serikali imechelewa kutuma fedha za kutoa huduma kwenye kaunti kwa muda wa miezi mitatu sasa.

 

 

 

 

 

KIMATAIFA

April 10, 2023