Waziri wa elimu Ezekiel Machogu, katibu wake Belio Kipsang pamoja na afisa mkuu mtendaji wa baraza la kitaifa la mitihani KNEC David Njegere hii leo wamefika mbele ya kamati ya elimu kujibu maswali kuhusiana na madai ya udanganyifu kwenye mtihani wa mwaka jana.
Machogu amedokeza kuwa madai hayo ni propaganda na kupuzilia mbali uvumi kwamba Kaunti za Kisii na Nyamira ndizo zilizokuwa na idadi kubwa zaidi ya watahiniwa waliopata matokeo bora kwenye mtihani wa KCSE.
Hali kadhalika Machogu amevilaumu vyombo vya habari kwa kusambaza simulizi hiyo aliyotaja kuwa ya uwongo.
Hata hivyo kamati hiyo imeelezea kamati hiyo imeelezea masikitiko yake kutokana na ukosefu wa mpango wa lishe shuleni.
In recognizing the crucial role of Parliament in holding the executive to account, I appeared before the departmental committee of Education chaired by Hon. Julius Melly.
I gave the address the current status of JSS,school feeding program, shortage of teachers, pic.twitter.com/DcAiOeEEgR— Hon.Ezekiel Machogu Ombaki, CBS (@machoguezekiel) April 13, 2023